Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba alizozitoa katika Husseinia al-‘Adhma Fatimiyya ya Najaf, alisema: Tunatoa shukrani na pongezi kwa muqawama wa Iraq kwa misimamo yao katika kukabiliana na ubeberuwa Kizayuni na Kimarekani ambao umevamia makao ya Hashdu Shaabi na kusababisha kuuawa kishahidi kwa vijana wetu wapendwa ndani ya vikosi hivyo.
Aliongeza kuwa: Tunawashukuru wananchi wote wa Iraq, hususan Ataba Tukufu ya Husseinia, kwa kuonesha mshikamano wao na watu wa Iran na Lebanon katika kuitikia wito wa Ayatollah Ali al-Sistani.
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf katika sehemu nyingine ya khutba yake alisema: Uamuzi wa Israel wa kunyonga wafungwa wa Kipalestina, pamoja na ukimya wa kimataifa mbele ya uchokozi huu wa kinyama, ni ukiukaji wa sheria zote za kimataifa na kibinadamu. Tunazitaka hasa jamii za kimataifa, Kiislamu na Kiarabu zipambane na sheria hii na ziwaonye kwa kunyongwa magaidi waliotiwa hatiani katika magereza yetu.
Hujjat al-Islam Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi kuhusu masuala ya kimataifa alisema: Baada ya maandamano ya mamilioni dhidi ya rais wa Marekani na kuondolewa kwa majenerali 12 akiwemo mkuu wa majeshi, pamoja na hasira ya kimataifa dhidi ya uamuzi wa vita dhidi ya Iran, kuna matarajio ya mapinduzi nchini Marekani; inshaallah hivi karibuni tunatarajia kusikia habari ya kutikisa ya kuanguka kwa serikali ya Donald Trump na kuvunjika kwa Marekani.
Pia aliishukuru Yemen kwa kuingia vitani na kwa kutoa wito wa kufungwa kwa Mlango wa Bab al-Mandab.
Katika sehemu nyingine ya khutba yake alisema: Wito kwa vijana wetu kujitolea unatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:
﴿إن الله اشتری من المؤمنین أنفسهم وأموالهم﴾
Na kwa mujibu wa yale tunayoyasoma katika Ziara ya Jamia Kabira ya Maimamu wetu (as): «ونصرتی لکم معدة» (Msaada wangu kwenu uko tayari).
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf aliendelea kusema: Kampeni ya kujitolea ina maana gani? Hii ina maana ya kutangaza utayari wa kuzuia uchokozi na kuleta ushindi kwa Uislamu pindi wito utapotolewa. Hapa ninawaomba vijana waaminifu wa Iraq wajitolee, wawe tayari kuutetea Uislamu na Ushia, na wawe tayari kuitikia wito huu.
Hujjat al-Islam Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi, akisema kwamba: ninawahakikishia kuwa Israel bila shaka itaangamia, Marekani itaanguka na itashindwa, aliuliza: Je, nafasi ya watu wa Iraq katika vita hii kubwa ni ipi? Tunakabiliwa na vita kubwa inayovuka mipaka na utaifa, tunakabiliwa na dalili za mwamko wa kimataifa, na dalili za kukaribia kudhihiri kwa Imamu wa Zama (as). Nafasi yetu ni ipi? Nafasi yetu ni maandalizi, utendaji wa kimedia, msaada wa kifedha na msaada wa kisiasa.
Kuhusu masuala ya ndani ya Iraq alisema: Kwa kuzingatia kupanda kwa bei, tunaitaka serikali ichukue hatua mara moja na kushughulikia suala hili; hivyo basi serikali inapaswa kuchukua msimamo thabiti haraka iwezekanavyo.
Aidha, aliipongeza timu ya Iraq kwa ushindi na kufuzu kwenda mashindano ya Kombe la Dunia, na akawatakia heri vijana wa timu hiyo ambao wameleta furaha kwa vijana na tabasamu katika nyuso zao.
Maoni yako